CRDB Microfinance Services Ltd: Wakulima wa Tumbaku

Wakulima wa Tumbaku

Picha zifuatazo zinaonyesha picha za wakulima wa tumbaku tulio watembelea mkoa wa Shinyanga.

Mkulima mkubwa kuliko wote kwa upande wa mkoa wa kitumbaku wa kahama Ndugu Safari Manjala wa kijiji cha Ulowa , kupitia chama cha msingi  Ilomelo akitolea vikonyo kwenye tumbaku yake. Ndugu Manjala kupitia tumbaku ameweza kujenga nyumba na kununua magari mazuri,anasomesha watoto  na pia ana mizigo.

Bi Rose Charles mkulima chama cha msingi Ibelansuha ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho akitoa vikonyo kwenye tumbaku yake na kuweka dawa ya kuzuia vikonyo. Kupitia tumbaku ameweza kujiendeleza kwa kiasi kikubwa ikiwamo kujenga nyumba ya kisasa na kusomesha watoto wake.

Ndugu Christopher Kabuga akipokea maelezo kutoka kwa wakulima wa kahawa wilayani Misenyi.

Siku ya kuuza tumbaku. Chama cha msingi NGOKOLO2001 wilayani kahama eneo la BUkomela. Wakulima wameweza kulipana zaidi
 ya sh 1600 kwa dola moja ya marekani kwa msimu wa 2013/2014.

Ukaguzi wa kuni chama cha maingi ngokolo.

 

Last Updated: Monday, 15 December, 2014